3 d - Translate

Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi ameshiriki Mkutano Mkuu Maalum wa CCM , uliofungwa rasmi na Mwenyekiti wa CCM Taifa , Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Dkt.Samia Suluhu Hassan leo tarehe 19 Januari 2025 katika Ukumbi wa Mkutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma.

Aidha, Dk.Mwinyi amethibitishwa na Mkutano huo Mkuu Maalum kuwa Mgombea wa Urais pekee wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi katika Uchaguzi mkuu mwaka huu.

Vilevile, Mkutano huo umemchagua Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa Mgombea pekee wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM na Dk.Emmanuel John Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza.

image