3 d - Translate

Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi ameshiriki Mkutano Mkuu Maalum wa CCM , uliofungwa rasmi na Mwenyekiti wa CCM Taifa , Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Dkt.Samia Suluhu Hassan leo tarehe 19 Januari 2025 katika Ukumbi wa Mkutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma.

Aidha, Dk.Mwinyi amethibitishwa na Mkutano huo Mkuu Maalum kuwa Mgombea wa Urais pekee wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi katika Uchaguzi mkuu mwaka huu.

Vilevile, Mkutano huo umemchagua Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa Mgombea pekee wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM na Dk.Emmanuel John Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza.

image
image
image
image
4 d - Translate

Actwazalendo
"Takwa la wananchi walio wengi Zanzibar hawataki kura ya siku 2 walilieleza 2020 hawakusilizwa na watu 21 wakauwawa sasa wanasema tena na sisi tunasimamia maamuzi yao juu ya jambo hili na tupo tayari kufa"

Source: ACT-Wazalendo Zanzibar

#tanzaniacommunitynetwork
#act-Wazalendo-Zanzibar

4 d - Translate

Ccm
Makamu Mwenyekiti CCM Zanzibar , Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi, akishiriki Mkutano Mkuu Maalum wa CCM Taifa unaofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma tarehe 18 Januari , 2025.

Mkutano huo umefunguliwa leo na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan.

#ccmtanzania

5 d - Translate

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akiongoza kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, kinachoketi leo tarehe 17 Januari 2025, Dodoma, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Mkutano Mkuu Maalum wa CCM utakaofanyika tarehe 18 na 19 Januari, jijini Dodoma.
#ccmtanzania

image
image
image
image
5 d - Translate

ACT
"Nilipata kusema na naendelea kusema huyu Bwana mdogo hawezi kuwa na uchungu wa Zanzibar kwa sababu hakukaa wala kusoma hapa na ndio maana ameshindwa kuitetea Zanzibar kuwa na mamlaka yake kamili" Ismail Jussa.
#zanzibarmpya
#zanzibarmoja
#mamlakamili.

About

Pata Habari kwa njia ya mtandao kupitia simu yako au computer yako ukiwa na Tanzania Community buree kabisa